1 Kings 7:1-12

Solomoni Ajenga Jumba Lake La Kifalme

1 aIlimchukua Solomoni miaka kumi na mitatu kukamilisha ujenzi wa Jumba lake la kifalme. 2 bAlijenga Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni, urefu wake ulikuwa dhiraa 100,
Dhiraa 100 ni sawa na mita 45.
upana wake dhiraa hamsini na kimo chake dhiraa thelathini,
Dhiraa 30 ni sawa na mita 13.5.
likiwa na safu nne za nguzo za mierezi zikishikilia boriti za mierezi zilizorembwa.
3Ilipauliwa kwa mierezi juu ya boriti zile zilizolala juu ya nguzo arobaini na tano, kumi na tano kwa kila safu. 4Madirisha yake yaliwekwa juu kwa safu tatu, yakielekeana. 5Milango yote ilikuwa na miimo ya mstatili, ilikuwa upande wa mbele katika safu tatu, ikielekeana.

6 eAkajenga ukumbi wa nguzo, ambao urefu wake ulikuwa dhiraa hamsini
Dhiraa 50 ni sawa na mita 22.5.
na upana wake dhiraa thelathini. Mbele ya jengo hilo kulikuwepo baraza. Mbele ya baraza kulikuwepo na nguzo na paa lililoningʼinia.

7 gAkajenga ukumbi wa kiti cha enzi, Ukumbi wa Hukumu, mahali ambapo angelitolea hukumu, akaufunika kwa mierezi kutoka sakafuni hadi darini. 8Kwenye jumba la kifalme ambamo angeliishi, aliiweka nyuma zaidi, ikiwa na mjengo wa aina moja na hiyo nyingine. Pia Solomoni akajenga jumba la kifalme linalofanana na huo ukumbi mkubwa kwa ajili ya binti Farao, aliyekuwa amemwoa.

9 hUjenzi huu wote, kuanzia nje mpaka kwenye ua mkuu na kuanzia kwenye msingi hadi upenuni, ulifanywa kwa mawe ya ubora wa hali ya juu yaliyokuwa yamechongwa kwa vipimo na kusawazishwa kwa msumeno nyuso zake za ndani na za nje. 10 iMisingi iliwekwa kwa mawe makubwa yaliyo bora, yenye urefu wa dhiraa kumi
Dhiraa 10 ni sawa na mita 4.5.
na mengine yenye urefu wa dhiraa nane
Dhiraa nane ni sawa na mita 3.6.
11Sehemu za juu kulikuwepo na mawe yenye ubora wa hali ya juu, yaliyokatwa kwa vipimo na boriti za mierezi. 12 lUle ua mkuu ulizungukwa na ukuta wa safu tatu za mawe yaliyochongwa na safu moja ya boriti za mierezi zilizorembwa, kama ulivyokuwa ua wa ndani wa Hekalu la Bwana na baraza yake.

Copyright information for SwhNEN